Miaka isiyozidi 50 kupita, tangu kifo cha Muhammad (mtume wa mwisho wa Uislamu) na mamlaka ya waislamu ilikuwa ina telezeka katika ufisadi, chini ya nasaba ya Ummayad, ya jeuri ya Yazid

Hussain ibn Ali, mjukuu wa mtume muhammad alichukua msimamo dhidi ya utawala haramu, wa Yazid. wakati Yazid alikuwa katika sehemu sawa, ya kuogofya na ya kudharauliwa kwa ukatili wake, Hussain alipendwa na kuheshimiwa na ujamii kwa jumla. Kwa hayo, Yazid aliamua kuwa yeye ataka kiapo cha utii kwa Hussain. kwa tamaa ya kupata uhalali wa utawala wake uliyorithi.

Msimamo wa Hussain dhidi ya dhuluma

Hussain alikuwa na uamuzi wa kufanya. kumkubali yazid, haimaanishi ni ujira mzuri, na maisha ya anasa. Kukataa kungekuwa sababu ya kifo chake mwenyewe. Anapaswa afanye nini? Wewe ungefanya nini? Au mimi ningefanya nini? Kwa Hussain uchaguzi kati ya jambo rahisi na jambo la haki, hauna hiari kabisa.

Hussain alikataa

Alisema: “Mimi sitampa mkono wangu yazid, kama mtu alifedheheshwa, wala sikimbii kama mtumwa… Mimi sikusimama kueneza uovu au kuwa na kiburi… Hamu yangu ni kuamrisha maadili mema na kuzuia mabaya” 

“Ninachotaka mimi ni kueneza maadili mema na kuzuia mabaya.”

- Hussain ibn Ali

Safari kutoka Makka kwenda Kufa

Maisha yake sasa chini ya tishio, Hussain waliamua kuhama yeye na familia yake, kwenda makka kwa matumaini kwamba mawakala wa Yazid, wata heshimu mji mtakatifu. Alipokuwa akisubiri, akifikiri hoja ingine ya pili, jumbe za msaada, zilianza kuwasili, kutoka nchi za utawala. Alianza safari kwenda Kufa, mji katika Iraq. Lakini, njia zilitekwa na kikosi cha askari wa Yazid, wakazifunga. Hussain na wafuasi wake, wali lazimika kuelekea mji wa jangwa la Karbala.

Walipo fika Karbala, jeshi liilizunguka kundi lao, na wamefunga njia ya kupatikana maji. Na kambi zote mbili kuwa Karbala, wapinzani waliwaandama. Hussain aliweka wazi kwamba hawezi kupiga magoti kwa Yazid. Jeshi pinzani la askari 30,000 ambalo ni kubwa mno kuliko, kundi la watu 72 la Hussain, na jamaa zake. Lilikuwa chini ya amri kali ya kutoruhusu Hussain kuondoka.

Baada ya wiki, habari ilimfikia Hussain, kwamba yazid ametuma amri kwamba Hussain haruhusiwi kuondoka Karbala mpaka aape kiapo cha utii. Mwisho ulikuwa inakaribia.

Mapa del viaje de Hussain ibn Ali de La Meca a Karbala

Ilustración del mapa de la batalla donde Hussain y su campamento habían sido rodeados por un ejército de 30.000 personas.

Msimamo wa mwisho wa Hussain ibn Ali

Usiku huo Hussain akekusanya kundi lake, akisisitiza kwao kwamba, Yazid alitaka maisha yake, wengine wote waweza kuondoka na kutoroka. Tena kutojipendelea kwa Hussain kumejitokeza. Hussain na familia yake na wenzake wote baada ya kunyimwa maji katika jangwa kali kwa siku tatu, Hussain akawaomba kundi lake kuondoka na kujiokoa.

Baada ya siku chache ya uadui huu, majeshi ya serikali waliagizwa kumshambulia na kumuua Hussain na wenzake. watu wa Hussain walikuwa wachache sana. Wakati wa vita ulianza. Watu wa Hussain, walipigana kwa ushujaa, kabla ya kuuawa, mmoja badaye ya mwingine.

Siku nzima, majeshi ya Yazid, walimtaka Hussain kutii, na HussAin alipinga. hatimaye, Hussain kabaki peke yake, bila mtu wa kumsaidia. Kwa kuchoka, na kiu, na majeraha mengi, Hussain akaanguka chini, huku wanawake na watoto wake wakiangalia.

Yeye pia aliuawa bila huruma, lakini alikufa akishikilia imara kanuni zake.

Ushindi wa Hussain, na msukumo wa urithi wake

Baada ya kifo cha Hussain, wanawake na watoto, walichukuliwa mateka. Dada yake Zainab, akachukua uongozi wa kundi hili, na alitoa hotuba baada ya hotuba, kulaani vitendo vya yazid na serikali yake, hadi kupambana nao kilele kwenye baraza la mtawala mwenyewe.

Zainab pengine ndie mtu wa kwanza, kuongozwa na msimamo wa Hussain, na kuutumia kama kichochezi cha mabadaliko. Yeye alikataa kushindwa au kuweka hofu, ili kuyachukulia majukumu hayo kwa maadili maovu ya waliohusika, katika jamii.

Licha ya ubaguzi wa kijinsia kuenea kwa jamii wakati huo, Zainab aliweza kuongoza na kuhamasisha wanaume na wanawake. Kwa mfano wa Hussain, kwamba mtu moja anaweza kusimama peke yake, didhi ya jeshi lamaelfu, ilimuongoza Zainab, katika hali ya kuweza adhibu na kuangusha msingi wa muaji ya utawala katika kasri yake kuweka msingi wa hatima ya Ummayad.

Leo mamilioni ya watu wanatoa heshima zao kwa Hussain ibn Ali kwa msimamo wake, na kuomboleza vita vya karbala ambapo, Hussain, familia yake na wenzake waaminifu waliuawa moja baadaye mwengine. Mahujaji wa kila jamii wanafika kwa ziara ya kaburi la Imam Hussain, kutoa heshima zao, huko Karbala, Iraq

karbala - día de ashura - arbaeen - imam hussain
Mamilioni ya watu kutoka kila pahali, wanatembelea mahali walipozikwa Hussain na wenzake.

marcha arbaeen - imam hussain - karbala - ashura
Karibu watu milioni 20-25, wanafika kwa ziara la kaburi ya Hussain siku ya ‘Arbaeen’ huu ni mkutano mkubwa wa amani namba moja, duniani