Ushindi wa Hussain, na msukumo wa urithi wake
Baada ya kifo cha Hussain, wanawake na watoto, walichukuliwa mateka. Dada yake Zainab, akachukua uongozi wa kundi hili, na alitoa hotuba baada ya hotuba, kulaani vitendo vya yazid na serikali yake, hadi kupambana nao kilele kwenye baraza la mtawala mwenyewe.
Zainab pengine ndie mtu wa kwanza, kuongozwa na msimamo wa Hussain, na kuutumia kama kichochezi cha mabadaliko. Yeye alikataa kushindwa au kuweka hofu, ili kuyachukulia majukumu hayo kwa maadili maovu ya waliohusika, katika jamii.
Licha ya ubaguzi wa kijinsia kuenea kwa jamii wakati huo, Zainab aliweza kuongoza na kuhamasisha wanaume na wanawake. Kwa mfano wa Hussain, kwamba mtu moja anaweza kusimama peke yake, didhi ya jeshi lamaelfu, ilimuongoza Zainab, katika hali ya kuweza adhibu na kuangusha msingi wa muaji ya utawala katika kasri yake kuweka msingi wa hatima ya Ummayad.
Leo mamilioni ya watu wanatoa heshima zao kwa Hussain ibn Ali kwa msimamo wake, na kuomboleza vita vya karbala ambapo, Hussain, familia yake na wenzake waaminifu waliuawa moja baadaye mwengine. Mahujaji wa kila jamii wanafika kwa ziara ya kaburi la Imam Hussain, kutoa heshima zao, huko Karbala, Iraq