Unaweza kudownload kwa tarakilishi (computa), vifaa mbalimbali, na kuvitumia vifaa hivi kwa matumizi ya Who is Hussain na kushiriki kampeni hii. Tutaendelea kubadili ukarasa huu uwe mpya, kila mara, kukusaidia zaidi na kazi hii. Fuata Twitter na Facebook, ikiwa kuna mabadiliko yoyote.

Faili yoyote, wewe utakubaliana na masharti yafuatayo: michoro iliyoko isibadilishwe hata kidogo; mafaili yoyote yasitumiwe kwa ajili ya matumizi yoyote, ila kampeni ya ‘who is hussain’. Bila ridhaa ya ‘who is hussain’ timu, vifaa vya ‘who is hussain’ haviruhusiwi kutumika.

Bango la vyombo vya habari – kijamii

Unaweza kujihusisha na kampeni kupitia mtandao (‘on line’ )na kupakua ‘avatars’ picha na mabango kwa ajili ya kugawanya katika majukwaa yote ya jamii, na vyombo vya habari. Inapatikana kwa kiingereza.

Mabango

Aina ya bango zimitolewa katika ukubwa wa A3, na DPI 300, na inayo mpaka ya cm1. Itapatikana kwa kiingereza, kifransa na kihispania.

Vipeperushi

Vipeperushi ni vya upande moja tu. Aina ya ukubwa A5, na dpi 300, pamoja na ya cm1. Ukubwa unaweza kubadilishwa vyovyote. Itapatikana kwa kiingereza, kifransa na kihispania.

Bendera za ukunjo

Mabango kwa ajili ya matukio. Faili za kubuni zimetolewa kwa ukubwa wa 25% shauri ya uchapaji, ukubwa wa (2000mm x 850mm) katika azimio 300dpi, na ukubwa pia unaweza kubadilishwa. Inapatikana kwa kiingereza, kifransa na kihispania.

Maandiko ya chupa

Hizi aina za maandiko za chupa zimetolewa katika 20 x 7.7cm na zimezidishwa kiasi 2cm (ambayo ukubwa unaweza kupunguzwa, ikihitajika. Na zitapatikana kwa kiingereza, kifransa na kihispania.

Kadi za salamu

Kadi za salamu, ambazo zina pande mbili, zimetolewa kwa ukubwa wa A5 kwa dpi 300 pamoja na mipaka ya cm 1. Zitaweza kupindwa kuwa ukubwa wa A6. Zipo na salaamu tofauti mbali mbali.

Alama za ‘who is hussain

Aina za alama zimetolewa katika azimio la juu, na miundo PNG. Zinafaa kuhamishwa katika miundo mbalimbali.

Mabango ya mtandaoni ‘online’

Ikiwa wewe unasimamia tovuti, utaweza kushusha na kufunga mabango yalioko tayari, kwa kuunganisha na whoishussain.org.

Kufungwa kwa ajili ya biashara

Bango hizi zimetolewa kuwekwa juu ya maduka, kwa kuonyesha biashara imefungwa kwa kuadhimisha siku ya Ashura.