Hussain ibn Ali alikuwa kiongozi mpinduzi katika karne ya saba ambaye ni wa mwisho kujitolea kwa haki za jamii katika ufisadi na udhalimu. Alijitolea kwa lolote, pamoja na maisha yake, kwa heshima ya wale walio karibu naye

Hussain ibn Ali alizaliwa mwaka 620 ad, katika familia, maarufu kwa maadili yao ya upendo, heshima na amani. iliyoinuliwa na babu yake Muhammad (mtume wa mwisho wa uislamu) Hussain alijulikana kwa uadilifu wake, ukarimu wa roho na upofu wa rangi, utangamano wa jamii. ni kwa sababu hii ndio watu kusongamana kwake na familia yake.

day of ashura - karbala - imam hussain
Hussain ibn Ali alizikwa katika mji wa Karbala, Iraq, ambapo wageni milioni huja kila mwaka, kutoe heshima zao kuu.

Hussain alikuwa mtu wa haki na heshima

Licha ya matarajio ya utamaduni wake kama ‘mkuu’ wa kabila lake na mfano mashuhuri katika dola ya Kiislamu, Hussain atajiepusha na ukuu wa cheo chake, na kupendelea kula pamoja na maskini na wahitaji. Alivunja tabia zote za kitamaduni, akaleta watu pamoja na kusaidia ambapo anaweza

Si muda mrefu kupita, baada ya muhammad kufariki, uongozi mkubwa wa milki ya Kislamu, ulifikia mikononi mwa wafisadi. Maadili mema, ambayo Muhammad, aliyafundisha maisha yake yote katika jamii polepole yaliondolewa na yazid, mtawala mpya, kutoka nasaba ya Ummayad, alidhihirisha kupata usimamizi kamili.

mourning - ashura - ashura day
Hussain ibn Ali anakumbukwa duniani kote, kama Ishara ya upinzani, aliye simama kwa maadili ya kibinadam.

Hussain alisimama makini, kwa haki za kijamii

Hussain alishuhudia haki za msingi na hadhi za watu wake zikiharibiwa, na maadili mema kutoka kwa jamii yake kuondolewa. Yazid alitawala kwa dhulma tu, na alitaka hussain atii na kuamini utawala wake.

Hussain alilazimika kufanya maamuzi, je aape kiapo chake cha utii kwa jeuri – na asimame kando, ingawa watu wanadhulumika? Au asimame na kuhatarisha maisha yake mwenyewe? Maneno aliyopata kwa babu yake yalikaririka katika moyo wake, na hussain akajuwa lipi la kufanya.

“Msimamo kuu, ni kusema neno la haki, kwa uso wa mjeuri”

Hussain alifanya sadaka ya mwisho

Hussain aliamua kusimama dhidi ya Yazid na alilazimika kuondoka mji wake, chini ya tishio la mauaji. Pamoja na familia yake na wenzake, Hussain walishika njia na kuelekea mashariki, kutafuta kupata msaada kwa ajili ya mapigano yake na kuepuka vurugo lolote. Ilikua katika safari hii, Hussain, familia yake na wenzake walilazimika kusimama na jeshi la zaidi ya 30,000, katika nchi tambarare na moto ya Karbala

Mwaka wa 680 ad, baada ya siku tatu bila maji wala chakula, na joto kali, Hussain, alisimama na akaanguka kwa ushujaa, kutetea wale walio karibu naye kutodhulumiwa, na wakati amesimama kwa kanuni zake. Kilichomfanya Hussain kusimama zaidi, ni kwamba yeye alichagua kusimama dhidi ya jeshi kubwa mno, licha ya kuwa na wenzi 72 tu pamoja naye.

“Kifo na utu, ni bora kuliko uhai wa udhalilishaji.”

– Hussain ibn Ali

Urithi ya Hussain inaendelea kuhamasisha

Kwa tendo hili la kutisha lakini la kujitolea kishujaa, Hussain hatimaye ulishinda, kifo chake kilikuwa kichochezi cha mabadaliko ya mapinduzi, na kilisababisha kuvunjika kwa utawala jeuri wa Yazid.

Kutoka kwa viongozi wa haki wa raia, kama Gandhi ambao ulitokana na msimamo wa Hussain, kujitolea katika misaada ya ndani – watu ulimwenguni kote walivutiwa na uongoza wa kutokuwa na ubinafsi, ujasiri na udhihirisho.

Historia ya Hussain ibn ali inasimamia kama msukumo kwa wote, bila kujali rangi au imani gani.