Ukarasa huu unajibu, baadhi ya maswali, kuhusu Hussain ibn Ali, msimamo wake, na umuhimu katika maisha yetu ya kisasa.

Historia ya Hussain ni kielelezo cha kwanza inayotukumbusha umuhimu wa kusimama dhidi, ya dhulma na ukorofi. Katika kila nchi na wakati, kwa kila taifa na kabila, historia ya Hussain inaleta msukumo na kutia moyo kwa watu: Kufahamu ukandamizaji na kuchukua hatua, hata uwe mdogo, kusema na kutenda dhidi yake. Je historia ya Gandhi na Martin Luther King yawahusu wahindi na wakristo pekee?

Kwa maneno yake mwenyewe, Hussain alifanya kwa haki matendo yake kwa hamu ya kugeuza taifa liwe bora: Kuhamasisha jamii kwa wema na kusimama dhidi ya uongo.

Msimamo wa hussein dhidi ya, majeshi ya Yazid ni hakika ya maisha, kwa sababu katika kila kizazi, kuna mdhulumu na mdhulumiwa. Utafiti wa maisha yake, na mfano, huhamasisha na humkumbusha mtu binafsi haja ya kujihusisha katika msimamo dhidi ya uonevu popote ulipo.

Watawala wa zama hizo walijaribu kuutoa msimamo wa Hussain kama alishindwa jaribio la waasi ili kupata nguvu kwake, na kuweka maenezi, ya kueneza ujumbe huu. Lakini, hii ilikuwa kuficha ukweli, ambao ulidhihirika kutokana na namna walivyomuuwa yeye na wenzake na familia yake.

Kueleza tabia zao sugu, walitengeneza hadithi, kwamba sababu halisi ya Hussain ya msimamo wake, ilikuwa kwamba Hussain akitafuta kuwa khalifa.

Kipimo cha mafaniko na kushindwa ulifanywa bora kupitia kwa muda mrefu. Yazid alitawala kwa miaka mitatu tu, na kwa leo husemwa kwa mbaya na kushutumiwa. Historia inaonyesha kuwa mshindi wa kweli ni Hussain, ambaye milele hukumbukwa kwa msimamo wake wa haki na ukweli.

Mwanafalsafa Søren Kierkegaard, aliiweka vyema, aliposema: “Jeuri akifa, utawala wake humalizika, shahidi akifa utawala wake huanza”

Unaweza kupata habari bure, kwa kujiandikisha hapa. Tutakutumia habari zaidi ya historia ya Hussain. tutakutumia barua pepe mara kwa mara, ujue zaidi kuhusu masuala mbalimbali kuhusiana na Hussain, msimamo wake na urithi wake inaoendelea.