Siku ya Ashura ni siku ya maadhimisho ya kifo cha Hussain ibn Ali, kiongozi wa mapinduzi wa karne 7, ambaye aliuawa katika vita vya Karbala. Siku ya Ashura inaomboleza na mamilioni kote duniani, kukumbuka Hussain, na msimamo wa ushujaa wake, kusimamia haki za jamii, dhidi ya jeuri na mafisadi, anayeitwa Yazid.

Historia ya Siku ya Ashura

Hussain ibn Ali alikuwa mjukuu wa muhammad (mtume wa mwisho wa uislamu), alizaliwa mwaka 620 ad katika familia maarufu kwa thamani yao ya upendo, heshima na amani. Hussain alikuwa kiongozi aliyejulikana sana kwa hurumayake, hekima na uadilifu. Si muda mrefu baada ya kifo cha muhammad, himaya ya kiislamu ilianza kuteleza katika migogoro ya kisiasa na ufisadi k wa Yazid (anayetoka nasaba ya ummayad) walichukuwa uongozi kwa nguvu na polepole akaanza kuharibu mfumo wa maadili ya jamii.

Hussain ibn Ali is buried today in the land of Karbala, Iraq, where millions of visitors come annually to pay homage to him.
Hussain ibn ali alizikwa katika ardhi ya Karbala, Iraq, ambapo mamilioni ya wageni huenda kila mwaka kufanya ziara yake.

Yazid alitaka Hussain aape, kiapo cha utii, ili kupata umaarufu kwa utawala wake wa kinyume cha sheria. Hussain kwa wajibu wa haki na heshima za kijamii, alikataa kufanya hivyo, licha ya kuwa ni hatari kwa maisha yake.

Hussain aliamua kuwa na msimamo, akaanza harakati ndogo, lakini ya nguvu. Aliamuwa kuacha faraji ya mji wake, na kuanza safari ya kuelekea Iraq. Hussain alisafiri na familia yake na wenzake 72, kwa kuweka wazi kwamba hakutaka fujo, ila alikuwa tayari kujitetea na kujitolea kivyovyote kwa mema ya watu wake.

Habari ilimfikia Yazid ya harakati ya Hussain na kwa hofu kwamba itazidi kupata kasi, Yazid alipeleka jeshi la watu 30,000 kumsitisha Hussain na wafuasi wake kwa miondoko yao. Walizuiwa kuondoka kwao hadi Hussain atoe kiapo, lakini Hussain alikataa. Yazid aliamuru jeshi lake kushambulia na kumuua Hussain na wafuasi wake, tarehe 10 ya mwezi wa kwanza wa kalenda ya kiislamu (muharram) – ambayo inajulikana kama Siku ya Ashura.

Ashura na vita vya Karbala

Illustration of the battle map where Hussain and his camp had been encircled by an army of 30,000.

Hussain na wafuasi wake walisimamishwa kwenye jangwa la Karbala, ambapo walinyimwa maji kwa siku tatu. Alfajiri ya Siku ya Ashura, Hussain na watu wake waliswali, wakijua kwamba kilichombele yao sasa ni kushindhwa, vivyo hivyo, walibaki imara na waaminifu kwa msimamo wao.

Vita vya Karbala vilianza saa sita za mchana. Makundi madogo yalitawanya kambi ya Hussain, kwenda kupambana kwa ushujaa na jeshi la Yazid. Mmoja baada ya mwingine, wafuasi wa Hussain walipigana na kuuliwa, hadi Hussain kutobaki na yeyote wa kumsaidia kwa wapinzani wake.

Hussain alichoka, alikuwa na kiu, na kujeruhiwa vibaya, kwa kupigana kishujaa na maadui zake, hadi kuanguka. Majeshi ya maadui, walimshambulia Hussain pande zote kwa panga, mikuki na mishale, mpaka mtu mmoja, kwa jina la shimr, kumkata kichwa kwenye ardhi moto ya Karbala.

Urithi kuhusiana Ashura

Wakati Hussain kauwawa kwenye vita, alikuwa mshindi kwa kifo chake. Vitendo na msimamo aliyofanya Hussain, huko Karbala, ulisababisha mfululizo wa fujo dhidi ya Yazid, ambayo hatimaye kusababisha kifo cha Yazid. Jeshi la Yazid waliwachukua wanawake na watoto, kutoka kambi ya Hussain, kama wafungwa wa kivita. Na walialekeya Syria kutoka Iraq, kama mateka.

Dadaake Hussain, Zainab na mwanawe Zain Al-Abideen, walimkaidi Yazid katika baraza lake, na hotuba maarufu ya Zainab na Zain Al-Abideen, ambayo iliwashangaza hata washirika wa karibu wa Yazid. Hapo hapo, na wafuasi wengine wa hussein, walieneza habari hii kuhusu mauaji na uhalifu uliofanyika Siku ya Ashura

Siku ya Ashura – siku ya maombolezo

mourning - ashura - ashura day
Hussain ibn Ali hukumbukwa dunia nzima kama ishara ya upinzani ambae alisimama kwa huruma.

Siku ya Ashura ni siku ambayo inakumbukwa na kuomboleza, na watu mamilioni duniani kote, kama siku ambayo Hussain na wafuasi wake waliuliwa katika vita ya Karbala. Leo, mahujaji kutoka duniani kote, huzuru, kaburi la Hussain, huko Karbala, ambako kazikwa, kutoa heshima zao kwa msimamo jasiri wa Hussain.

Siku ya Ashura waislamu wengi wanashirika kwenye mikusanyiko mikubwa ya amani, ambapo wanasoma mashairi, ya kumbukumbu Hussain, huku wakiwalaumu na kuonyesha kero zao, kwa kupiga vifua vyao, kufuatana na mila za kiutamaduni. Wengi huchukulia Siku ya Ashura siku ya kufanya matendo ya huruma na sadaka kama njia ya wao kuweka hai kanuni Hussain alizojitolea nazo.