Who is Hussain, ni shirika la kimataifa, lililoazimia kujulisha duniai nzima kuhusu mtu mtakatifu, ambaye jina lake Hussain, na kaishi miaka 1400 iliyepita.

Lengo letu ni kuhamasisha wananchi kuwa mfano wa Hussain na kuleta mabadiliko mazuri duniani. Wawakilishi wetu wanaojitolea huchangi utoaji wa damu, kulisha wasio na makazi na mengi zaidi.

Ni nani sisi

Mwaka 2012 tulikuwa kundi la vijana kutoka jamii mbalimbali, hapa London. Pamoja, tuliongozwa na msimamo wa Hussain, kwa mfano wake tuliamuwa kusaidia na kuchangia jamii. Sisi, tuligunduwa kwamba, dunia tunayoishi imezidiwa na ubinafsi kuliko kibinadamu. Hisia za huruma, zilikuwa zina kufa. Kutatua hili, tulitaka tushiriki, msukumo wa Hussain kwa wote.

who is hussain - vancouver - blood donation

Tulitaka Hussain ibn ali kuwa mfano wa kuigwa na wote, bila kujali jinsia,dini, tabaka, imani, au chochote kinachobagua ubinadamu. Hussain alijali zaidi, uelewano wa kibinadamu, kuliko majina au cheo, vinayvobagua watu. Na kwa sababu hii, tunasisitiza, kwamba sisi sio watu wa dini au kisiasa au chochote chengine ambacho kinagawanya watu wengine wote.

Tangu mwanzo, tulipenda msimamo wa hussain, na tulianza kampeni hii duniani kote. Tunaongezeka. Kundi letu ni watu binafsi, kutoka tamaduni nyingi, lugha, dini, utaifa na matabaka ya jamii mbali- mbali. Msimamo wetu ni kuleta mabadiliko mema, kwa kufuata mifano ya Hussain ibn Ali.

Kwa kujitolea duniani kote, kuandaa uchangiaji wa damu, kusambaza chakula kwa wale wanaohitaji, kujitolea katika kutoa misaada, tumejitaidi kwa vitendo kuliko maneno na yote kwa jina la Hussain. Bado kuna mambo mengi ya kufanya.

Je nani ni wafuasi na wafadhili wetu?

Who is Hussain haina uhusiano na mashirika mengine yoyote, ila kufanikisha kwa kampeni hii, tumetegemea hiari za watu wengi, hapa uingereza na pia duniani kote. Timu ya Who is Hussain inapenda kuwashukuru wote waliotoa msaada. Ikiwa ungependa kujiunga na kampeni hii, tupelekee barua pepe, au soma ukurasa wa matukio yetu.