Mara kwa mara uliza maswali kuhusu ushirika Who is Hussain – ni nini? Sisi ni nani? Na tunataka nini? Kama ufatavyo, ikiwa swali lako halikufanikiwa, tafadhali wasiliana nasi hapa.

Who is Hussain ni shirika la kimataifa lililojitolea kujulisha ulimwengu kuhusu mtu mtakatifu aliyeishi miaka 1400 iliyopita. Mtu aitwaye Hussain. Lengo letu ni kuhamasisha wananchi kuwa mfano wa hussain na kuleta mabadiliko mazuri duniani. Wawakilishi wetu wanaojitolea huchangi utoaji wa damu, kulisha wasio na makazi na mengi zaidi.

Lengo letu ni kuhamsisha watu kwa kusaidia jamii zao, ambayo jamii hiyo iliwapa mengi, na kufanya mabadiliko mazuri katika jamii, na tunaona kwamba maisha ya Hussain, ni mahali manufaa kuanzia. Kila mtu anajua kwamba kufanya wema ni jambo la haki, ila sisi sote, wakati mwingine, tuna haja ya uchochezi wa kutuamsha, inabidi tusukumwe.

Maelfu ya watu ambao wanaohusika na kampeni hii, tangu ilipoanza, walisukumwa na msukumo wa Hussain.

Tunaamini kwamba Hussain tu ndiye anaweza kukupa msukumo huu. Ikawa kila mtu anasoma tovuti hii sasa, kaleta hata badiliko dogo zuri katika maisha yake, au kafanya mchango mdogo, kwa jamii, kutokana na msukumo wa Hussain, tutafikiria mafanikio makubwa mno.

Sisi tunataka, wewe uchukue muda kidogo ujifikirie kwamba kutokana na msimamo wa Hussain, utajitolea nini kusaidia jamii karibu nawe.